Napoli watwaa ubingwa wa Serie A kwa mara ya nne

Napoli walimaliza msimu kwa pointi 82,alama moja mbele ya AC Milan.

Dismas Otuke
1 Min Read

Napoli ndio mabingwa wa ligi kuu nchini Italia Serie A msimu wa mwaka 2024-2025, baada ya kuwashinda Cagliari mabao 2-0, katika mechi ya kufunga msimu jana usiku uwanjani Diego Armando Maradona.

Mabao ya Scott McTominay, na Romelu Lukaku, yaliwapa Napoli ushindi wa taji ya nne ya Scudetto.

Inter Milan pia walipata ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Como,ingawa haikutosha kuhifadhi taji.

Napoli walimaliza msimu kwa pointi 82,alama moja mbele ya AC Milan.

Napoli wameshinda taji hiyo miaka 1986-1987, 1989-1990, 2022-2023 na 2024-2025.

Juventus wameshinda ubingwa huo Serie A mara 36, wakifuatwa na Inter, kwa mataji 20, huku AC Milan wakishinda 19.

Share This Article