Nairobi United wanusia hatua ya makundi Kombe la Shirikisho

Dismas Otuke
1 Min Read

Klabu ya Nairobi United imejikatia tiketi kwa mchujo wa mwisho, kabla ya hatua ya makundi kuwania Kombe la Shirikisho Afrika, baada ya kuibandua timu ya National Enterprises Corporation (NEC) FC kutoka Uganda kwa mabao ya ugenini.

Nairobi United imetoka sare ya bao 1-1 katika marudio ya mchujo wa kwanza   Jumamosi ugani Nyayo, lakini wakasonga mbele baada ya kutoka sare ya 2-2 nchini Uganda wiki jana, mechi ikimalizikia kwa sare ya 3-3.

Wageni NEC walichukua uongozi dakika ya 26 kupitia kwa Charles Waibi, kabla ya wenyeji kusawazisha dakika ya 65 kupitia kwa Duncan Omala.

Timu hiyo inayofadhiliwa na kaunti ya Nairobi itachuana na mshindi kati ya Madani ya Sudan na Etoile du Sahel kutoka Tunisia, katika mchujo wa mwisho huku mshindi akifuzu kwa hatua ya makundi.

United wanashiriki kombe la Afrika kwa mara ya kwanza baada ya kutwaa kombe la Mozzart Bet msimu jana, na pia wamepandishwa ngazi kushiriki ligi kuu kwa mara ya kwanza msimu huu .

 

Share This Article