Klabu ya Nairobi United ndio waakilishi rasmi wa Kenya katika mashindano ya kombe la Shirikisho msimu ujao.
Hii ni baada ya timu hiyo inayofunzwa na kocha Nicholas Muyoti, kuwalemea Gor Mahia mabao 2-1, katika fainali ya kombe la Mozzart Bet siku ya Jumapili uwanjani Ulinzi.
Nairobi United wanaofadhiliwa na serikali ya kaunti wamekuwa na msimu wa kufana baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi ya NSL, na kupandishwa kushiriki ligi kuu FKF PL msimu ujao kwa mara ya kwanza.
Hata hivyo mtihani ulio mbele ya Nairobi United ni mgumu wakihitaji kusajili wachezaji wenye haiba kuu watakowawezesha kufanya vyema ligini na hata mashindano ya Afrika.