Aliyekuwa Naibu Rais wa Afrika Kusini David Mabuza, aliaga dunia jana akiwa na umri wa miaka 64.
Mabuza alihudumu katika wadhfa wa Naibu Rais kwa muhula mmoja kati ya mwaka 2018 na 2023, na pia kama Naibu kiongozi wa chama cha African National Congress( ANC) baina ya mwaka 2017 na 2022.
Marehemu alifariki akipokea matibabu katika hospitali moja nchini Afrika Kusini.
Mabuza alichangia pakubwa kwa kuchaguliwa kwa Rais Cyril Ramaphosa mwaka 2017, kabla ya kujiuzulu mwaka 2023 na kujitokeza tena wakati wa uchaguzi wa mwaka jana.