Mzozo kati ya Rais na Wabunge watokota

Kama kile kinachoonekana kuwa vita vya kibabe, pia Rais amebuni jopokazi lenye asasi 11 kuimarisha vita dhidi ya jinamizi la ufisadi nchini.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mzozo kati ya Rais William Ruto na Wabunge kutoka mabunge yote mawili; Seneti na Bunge la Kitaifa, unaonekana kuchukua mkondo mpya huku pande zote zikikaa ngumu.

Maseneta na Wabunge mnamo siku ya Jumanne walitishia kuwatimua Maspika wote wawili kwa kushindwa kulinda taasisi hizo dhidi ya kushambuliwa na Rais.

Aidha, Wabunge walimtaka Spika Moses Wetang’ula kumuita Rais Ruto bungeni ili kuthibitisha madai yake kuwa wabunge wa kamati hupokea mlungula ili kupitisha miswada.

Kama kile kinachoonekana kuwa vita vya kibabe, pia Rais amebuni jopokazi lenye asasi 11 kuimarisha jitihada za kukabiliana na jinamizi la ufisadi nchini.

Matamshi ya Ruto yalionekana kuwaguza mishipa baada ya kudai kuwa wabunge wa kamati hupewa kiinua mgongo cha hadi shilingi milioni 10 ili kupitisha miswada.

Share This Article