Mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga, umepelekwa katika majengo ya Bunge mapema Ijumaa, kabla ya kupelekwa uwanjani Nyayo kwa mazishi ya kitaifa.
Wabunge na watu maarufu ambao hawakupata fursa ya kuutazama mwili wa marehemu na kutoa heshima zao za mwisho wamemiminika katika majengo ya bunge.
Mwili wa Raila ulikuwa uwasilishwe bungeni Alhamisi baada ya kuwasili kutoka India, lakini mpango huo ukabadilishwa na badala yake kupelekwa katika uwanja wa michezo wa Moi Kasarani, ambapo wananchi waliutazama na kutoa heshima zao mwisho.
Mazishi ya kitaifa katika uwanja wa michezo wa Nyanyo, inatarajiwa kuchukua muda wa masaa mawili.
Raila Odinga atazikwa Jumapili nyumbani kwake Bondo, kaunti ya Siasa.