Mwenyekiti wa Basketiboli nchini (KBF) Paul Otula, afariki

Dismas Otuke
1 Min Read

Mwenyekiti wa shirikisho la mpira wa kikapu nchini -KBF,Paul Otula, ameaga dunia .

Mara ya mwisho kwa Otula kuonekana kwenye hafla ya michezo ilikuwa ni kwenye uchaguzi wa kamati ya Olimpiki NOCK.

Kulingana na familia yake ,marehemu alipatwa na mshtuko wa moyo akiwa nyumbani kwake Nairobi.

Mwili wake umepelekwa katika chumba cha Lee Funeral.

Otula aliyezaliwa mwaka 1964, katika kaunti ya Homabay,amekuwa mwenyekiti wa KBF, tangu mwaka 2010 na alichaguliwa tena kwa muhula wa mwisho mwaka 2021.

Otula pia amekuwa mwanachama wa kamati kuu ya NOC-K.

Aidha Otula, amekuwa Mwalimu mwandamizi wa shule za upili za Mangu,Maseno na Nairoibi Sunshine.

Share This Article