Mwanariadha Rebecca Cheptegei azikwa nyumbani Uganda

Dismas Otuke
1 Min Read

Mwanariadha wa Marathon Rebecca Cheptegei aliyeuawa kinyama na mpeinziwe katika kaunti ya Trans-Nzoia, amezikwa kijeshi Jumamosi kijijini Kapsiywo wilaya ya Bukwo mashariki mwa Uganda.

Mazishi hayo yaliongozwa na wanajeshi huku waombelezaji wengine waliohudhuria wakivalia mashati tao ya kulaani dhuluma za kijinsia .

Wanariadha wenza wa Uganda ,maafisa wa shirikisho la riadha nchini humo na marafiki walichangisha zaidi ya shilingi laki nne za Kenya .

Marehemu Cheptegei alifariki baada ya kuteketezwa na mpenziwe wa zamani kwa kutumia petroli punde baada ya kurejea kutoka Paris Ufaransa ,aliposhiriki marathon katika michezo ya Olimpiki ya mwaka huu.

Share This Article