Mwanamuziki wa Uganda akamatwa nchini China

Grenade alisafiri kuelekea China kama mtalii, alipofika huko akatumbuiza kwenye tamasha bila kibali cha kazi.

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamuziki wa Uganda Deus Nduggwa maarufu kama Grenade Official alikamatwa nchini China, habari zilizotolewa kupitia akaunti yake ya Instagram bila maelezo ya kina.

Grenade alisafiri hadi China na Joram Mukisa ambaye sasa anaelezea kwamba alikamatwa kwa kuendesha biashara nchini humo huku akitumia Visa ya utalii.

Inaripotiwa kwamba mwanamuziki huyo alifanikiwa kupata kazi za kutumbuiza nchini China ambapo aliingia kama mtalii. Joram alichapisha video inayomwonyesha akitoa maelezo ambapo alisema Grenade aliandaa tamasha jijini Guangzhou kabla ya kukamatwa.

Kulingana na Joram, Grenade alihitaji kibali cha kufanya kazi nchini China ili akubaliwe kutumbuiza nchini humo.

“Niko hapa China. Tuliingia China na Grenade kwa biashara ya kawaida ikitizamiwa kwamba hii ni nchi ya biashara” alielezea Joram kwenye hiyo video.

Anaendelea kusema jinsi waandaaji wa matamasha walimpa mwenzake fursa za kutumbuiza ili ajipatie pesa na walifaikiwa kutumbuiza jijini Guangzhou.

Joram ana imani kwamba Grenade ataachiliwa hivi karibuni.

Share This Article