Polisi mapema Jumapili wamemnasa mwanamke mmoja aliyekuwa na misokoto 154, ya bangi katika kaunti ya Bungoma.
Polisi waliokuwa wamearifiwa na umma walivamia nyumba ya mshukiwa huyo kwa jina Beatrice Nekesa Wafula, katika kijiji cha Nabuloli, na kupata bangi hiyo.
Mshukiwa alipelekwa katika kituo cha polisi cha Sirisia, akisubiri kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka.