Mwanaharakati Boniface Mwangi aachiliwa kwa dhamana

Martin Mwanje
1 Min Read
Mwanaharakati Boniface Mwangi akiwa mahakamani

Mwanaharakati Boniface Mwangi ameachiliwa kwa dhamana binafsi ya shilingi milioni moja.

Hii ni baada ya kukanusha mashtaka ya kumiliki silaha bila cheti halali na pia kupatikana na vitoza machozi vitatu.

Kesi dhidi yake itatajwa Agosti 19.

Awali, Mwangi alipangiwa kushtakiwa kwa kuwezesha vitendo vya kigaidi lakini mashtaka hayo yaliondolewa.

Mshukiwa huyo alikamatwa nyumbani kwake huko Lukenya, kaunti ya Machakos juzi Jumamosi.

Idara ya Upelelezi wa Jinai, DCI ilielezea kwamba anahusishwa na uwezeshaji wa vitendo vya kigaidi wakati wa maandamano ya Juni 25, 2025.

“Wakati wa kukamatwa kwake, maafisa walichukua simu mbili za rununu, kipakatalishi na vitabu kadhaa vya kuandika,” ilisema DCI kwenye taarifa.

Wapelelezi hao walisema baada ya kumaliza kutoka nyumbani kwake, walimpeleka Mwangi kwenye afisi yake ya Mageuzi Hub kwenye barabara ya Rose Avenue mtaani Hurlingham.

Baada ya kusaka afisi hiyo, maafisa hao waliondoka na diski tisa za kuhifadhi data, vipakatalishi viwili, sili za kampuni za Brave Media na Courage, muhuri wa kampuni, vitabu sita vya hundi, nakala za hati za ushuru, makopo mawili ya gesi ya kutoza machozi na vingine.

Tangu kukamatwa kwake, Mwangi amezuiliwa katika kituo cha polisi cha Pangani akisubiri kufikishwa mahakamani.

Share This Article