Aliyekuwa mwaniaji kiti cha Urais nchini Kenya mara mbili, Mwalimu Mohammed Abduba Dida, ameachiliwa na gereza la Marekani baada ya kukamilisha kutumikia kifungo cha miaka mitatu.
Dida alitarajiwa kuachiliwa kutoka gerezani Aprili 3 mwaka 2029, baada ya kutumikia kifungo cha miaka saba, lakini hukumu hiyo ikapunguzwa hadi miaka mitatu .
Dida atatumikia jamii kwa kifungo cha nje kilichosalia cha miaka minne nchini Marekani, baada ya kuachiliwa huru kutoka gereza la jimbo la Illinois.
Dida amekuwa kwenye gereza hilo tangu Novemba 18 mwaka 2022, baada ya kupatikana na hatia ya kumvizia na kumtishia mkewe wa zamani ambaye ni raia wa Marekani.