Muungano unaotawala nchini Japani wapoteza wingi wa viti katika Baraza la Juu la Bunge

Ni mara ya kwanza katika historia ya miaka 70 ya LDP kuongoza muungano ambao hauna udhibiti kwenye mabaraza yote mawili ya bunge.

Martin Mwanje
1 Min Read
Ishiba Shigeru - Waziri Mkuu wa Japani

Muungano unaotawala nchini Japani umepoteza wingi wake wa viti katika Baraza la Juu la Bunge kufuatia uchaguzi uliofanyika Julai 20.

Akizungumza na vyombo vya habari Julai 20, Waziri Mkuu Ishiba Shigeru ameashiria kuwa anakusudia kubaki katika wadhifa wake.

Muungano huo ulihitaji kushinda viti vipya 50 ili kuendelea kudhibiti baraza hilo.

Hata hivyo, chama cha Liberal Democratic, LDP, na mshirika wake Komeito vimepata viti 47, na kupungukiwa idadi hiyo.

Ni mara ya kwanza katika historia ya miaka 70 ya LDP kuongoza muungano ambao hauna udhibiti kwenye mabaraza yote mawili.

Share This Article