Gavana wa Tharaka, Muthomi Njuki, amechaguliwa Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Magavana.
Magavana walimchagua Njuki, katika mkutano ulioandaliwa kujadili kuhusu nyumba za gharama nafuu na bima ya afya ya jamii (SHA), mjini Naivasha kaunti ya Nakuru.
Huku akikubali wadhifa huo, Gavana njuki aliwashuruku wenzake kwa kuwa na imani naye, akitaja uchaguzi huo kuwa wa hadhi ya juu.
“Nitazingatia maadili ya afisi na kushirikiana katika kuboresha ajenda za Baraza hili,” alisema Njuki.
Njuki anachukua wadhifa huo ambao awali ulishikiliwa na Gavana wa Nyeri Mutahi Kahiga, ambaye alijiuzulu mwezi Oktoba kuhusiana na matamshi aliyoyatoa baada ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga.