Tume ya uchaguzi nchini Malawi NEC imemtangaza rasmi Rais wa zamani Peter Mutharika kuwa mshindi wa uchaguzi wa Urais, baada ya kupata kura milioni 3,035,249, ikiwa asilimia 56.8 ya kura zilizopigwa.
Professa Arthur Peter Mutharika na makamu Rais wake Jane Ansah wa chama cha Democratic Progressive ndio Rais na Naibu Rais wateule.
Mutharika, aliye na umri wa miaka 85, anarejea katika Ikulu baada ya kubwagwa na Rais anayeondoka, Lazarus Chakwera miaka mitano iliyopita.
Wafuasi wa Mutharika wamefurika barabarani mjini Lilongwe na Blantyre kusherehekea ushindi huo.