Professa Arthur Peter Mutharika ameapishwa siku ya Jumamosi kuwa Rais wa Malawi kwa kipindi cha miaka mitano ,akihudumu kwa muhula wa pili.
Rais William Ruto aliwakilishwa na waziri wa Michezo na masuala ya vijana Salim Mvurya kwenye halfa hiyo ya uapisho huo.
Akihutubia taifa punde baada ya kula kiapo Mutharika amesema alikubali matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 na Lazarus Chakwera kutokana na imani yake na kuheshimu katiba ya nchi.
Mutharika aliye na umri wa miaka 86 alishinda uchaguzi wa Urais baada ya kuzoa asilimia 56,8 ya kura dhidi ya mtangulizi wake Chakwera aliyepoata asilimia 33 .