Museveni athibitisha uteuzi wa majaji

Majaji hao 11, wamekuwa wakihudumu kama makaimu katika mahakama kuu tangu mwaka 2023.

Marion Bosire
1 Min Read

Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni, amethibitisha uteuzi wa Majaji kumi na mmoja wa Mahakama Kuu.

Majaji hao, ambao awali waliteuliwa mwaka 2023 kwa kipindi cha miaka miwili kwa msingi wa uteuzi wa muda, sasa wamethibitishwa rasmi baada ya kumaliza muda wao kwa mafanikio.

Nyaraka za uteuzi zilisainiwa na Rais tarehe 24 Agosti, 2025.

Majaji hao 11 ni pamoja na Jaji Makumbi David Samson Lwokya, Jaji Rubagumya Tumusiime Patience, Jaji Kania Rosette Comfort, Mheshimiwa Jaji Naluzze Aisha Batala, na Jaji Mwaka Philip Willibrord.

Wengine ni, Jaji Jacqueline Mwesigwa, Jaji Dkt. Akello Echookit Christine, Jaji Karemani Jamison Karemera, Jaji Farouq Lubega, Jaji Kwizera Amos, na Jaji Nabakooza Flavia.

Katika tarehe hiyo hiyo, Rais pia aliteua wasajili watatu wa Idara ya Mahakama.

Watatu hao ni Agnes Alum, Tusiime Sarah Bashaija Barungi, na Justine Atukwasa ambao wamekuwa wakihudumu katika Idara ya Mahakama kama Manaibu Wasajili.

Share This Article