Murkomen: Serikali haitalegeza kamba kwenye mashtaka ya ugaidi dhidi ya waandamanaji

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri wa Usalama wa Taifa Kipchumba Murkomen anza ziara ya Jukwaa la usalama kaunti ya Uasin Gishu.

Waziri wa Usalama wa Taifa Kipchumba Murkomen, amesema serikali haitalegeza kamba kwenye mashtaka ya ugaidi dhidi ya waandamanaji waliotiwa nguvuni.

Akizungumza Eldoret, alipoanza ziara ya Jukwaa la Usalama  katika kaunti ya Uasin Gishu, waziri huyu aliikosoa Chama cha Wanasheria nchini (LSK), kwa kuegemea upande wa wahalifu na wala sio upande wa wananchi wanaozingatia sheria na ambao walipoteza mabilioni ya pesa wakati wa maandamano yaliyoshuhudiwa kote nchini.

“Sheria kuhusu uzuiaji wa ugaidi ni bayana. Kuzua ghasia na kuhatarisha maisha , uharibifu wa mali, utumizi wa silaha na vilipuzi na kuhujumu utoaji wa huduma muhimu, ni makosa ya kigaidi,” alisema Murkomen.

Murkomen alisema mahakama haiwezi kutolewa vitisho ili kulegeza dhamana kwa wale walioshtakiwa kwa makosa ya ugaidi.

Alitoa wito kwa mwenyekiti wa LSK  Faith Odhiambo, kuunga mkono uzingatiaji wa sheria, unaojumuisha kuwafungulia mashtaka wahalifu.

Share This Article