Mudavadi kufungua rasmi ubalozi wa Kenya nchini Morocco

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri mwenye mamlaka makuu Musalia Mudavadi.

Waziri mwenye Mamlaka Makuu aliye pia Waziri wa Mambo ya Nje Musalia Mudavadi, anatarajiwa kufanya ziara rasmi ya siku tatu nchini Morocco.

Lengo kuu la ziara hiyo ya Mudavadi ni ufunguzi rasmi wa ubalozi wa Kenya Jiji Rabat, unaonuia kuimarisha uhusiano wa nchi hizi mbili.

“Mudavadi anatarajiwa kufungua rasmi ubalozi wa Kenya Jijini Rabat uliofunguliwa Disemba mwaka 2023 kama sehemu ya kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Kenya na Morocco,” alisema Jacob Ngetich, Mkurugenzi wa mawasiliano katika afisi ya Mudavadi.

Ng’etich alidokeza kuwa Mudavadi atashiriki mkutano wa pande mbili na Aziz Akhannouch, Mkuu wa Serikali aliyepia Waziri Mkuu wa Morocco.

Pia, atapigia debe kuimarishwa kwa usawa wa kibiashara ambao sasa unaipendelea Morocco.

“Kenya huuza nchini Morocco majami Chai, Kahawa, Matunda za thamani ya shilingi Milioni 480, huku Morocco ikiuza humu nchini Mbolea, mafuta na vipuri vya ndege vya thamani ya shilingi bilioni 12.1,” alisema Ng’etich.

Katika ziara hiyo, Mudavadi atapata fursa ya kukutana na Waziri wa Kilimo na biashara kwa mazungumzo.

Share This Article