Mudavadi: Kenya inatafuta wawekezaji katika sekta ya uchimbaji madini

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri wa Mambo ya Nje Musalia Mudavadi akutana na balozi wa Australia nchini Marekani Kevin Rudd, Jijini Washington DC.

Waziri mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi, amesma Kenya inatafuta wawekeza walio na uzoefu na uwezo wa kifedha ili kuchimba madini ya hapa nchini na kuboresha thamani yake ya taifa.

Akizungumza alipokutana na balozi wa Australia nchini Marekani Kevin Rudd Jijini Washington, Mudavadi ambaye pia ni waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, alisema taifa hili litashirikiana na kampuni za uchimbaji madini zilizo na uzoefu, ambazo pia zitatoa mafunzo kwa wakenya jinsi ya uchimbaji madini kwa njia salama ili kuimarisha maisha ya jamii hasaa katika eneo la Mrima Hills kaunti ya Kwale.

“Huku eneo la pwani ya Kenya likiwa na madini ya kipekee, Kenya itashirikiana na kampuni ambazo zitazingatia uhifadhi wa mazingira, kukumbatia mbinu bora za kimataifa na zitakazo hakikisha ardhi imerejeshwa lkatika hali yake ya awali baada ya uchimbaji madini,” alisema Mudavadi.

Kwa upande wake balozi Rudd, alirejelea kuwa kampuni za Australia, zina uzoefu wa zaidi ya karne moja za uchimbaji madini na zenye rekodi bora katika uhamasishaji wa jamii.

Share This Article