Mudavadi amkabidhi Cheptumo wizara ya Jinsia, Sanaa na Utamaduni

Tom Mathinji
1 Min Read
Mudavadi amkabidhi waziri Cheptumo wizara ya jinsia, Sanaa na Utamaduni.

Waziri mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi leo Ijumaa amekabidhi wizara ya Jinsia, Sanaa na Utamaduni kwa waziri mpya aliyeteuliwa, Hanna Wendot  Cheptumo.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mudavadi alimtakia Dkt. Cheptumo mafanikio katika jukumu lake jipya, akisema kwamba anatazamia kumuona akipandisha hadhi wizara hiyo ili Wakenya waweze kunufaika na kazi yake.

Waziri huyo wa Mambo ya Nje, aidha alielezea umuhimu wa wizara hiyo katika kuimarisha usawa wa kijinsia, utamaduni, turathi na Sanaa.

“Wizara hii hutekeleza jukumu muhimu katika kukuza sera zitakazoboresha usawa wa kijinsia, kudumisha utadamuni na kukuza sanaa,” alisema Mudavadi.

Kwa upande wake, Cheptumo alimshukuru Mudavadi kwa uongozi wake katika wizara hiyo, huku akitoa ahadi ya kuendeleza mafanikio yaliyoafikiwa, akithibitisha kujitolea kwake kuendeleza usawa wa kijinsia, kusaidia sekta ya ubunifu, na kuhifadhi turathi za utamaduni wa humu nchini.

Mudavadi amekuwa akihudumu kama kaimu katika wizara hiyo kwa muda wa miezi tisa.

Share This Article