Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi amefungua rasmi Kikao cha Saba cha Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Kenya na Iran.
Ufunguzi huo ulifanyika jijini Nairobi leo Jumanne.
Mudavadi ametaja kikao hicho kama hatua muhimu kuelekea kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili na pia kupanua mipaka ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
“Ushirikiano wetu unazidi ari ya kudumisha ushirikiano wetu uliopo kwa sasa; unahusu kufungua fursa mpya na kuboresha uhusiano wetu hadi kufikia upeo mpya,” alisema Mudavadi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje.

“Katika kikao cha hii leo, tulipitia upya hatua zilizofikiwa na kutafuta njia mpya katika nyanja zinazochipukia kama vile kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi, utengenezaji bidhaa, uchukuzi na miundombinu, elimu na mafunzo, uhusiano wa forodha hadi forodha, na nishati mbadala, miongoni mwa zingine.”