Mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne, KCSE umekamilika leo Ijumaa huku Wizara ya Elimu ikisema visa vya wizi wa mtihani huo vimepungua pakubwa.
Katibu wa Idara ya Elimu ya Msingi Dkt.Belio Kipsang alisifia kupungua kwa wizi wa mtihani huo na hatua ya kuwa nambari maalum kwa kila mwanafunzi katika karatasi za mtihani, pamoja na kubuniwa kwa kundi la maafisa wa asasi mbalimbali.
Dkt. Kipsang amepongeza kundi la maafisa wa asasi mbalimbali kwa kuzuia tovuti ambazo awali zilitumika katika wizi wa mtihani.
Hata hivyo, amesema visa vichache viliripotiwa vya watu kujisingizia kuwa watahiniwa, hasa katika shule za kibinafsi kaunti ya Nairobi.
Watahiniwa 965,501 walifanya mtihani wa KCSE mwaka huu, hili likiwa ni ongezeko la watahiniwa 66,048 ikilinganishwa na idadi ya mwaka 2023.