Mtanzania Dkt Faustine Ndugulile ataeuliwa Mkurugenzi WHO Afrika

Dismas Otuke
1 Min Read

Dkt Faustine Ndugulile wa Tanzania amechegauliwa Mkurugenzi wa ukanda wa Afrika katika Shirika la Afya Ulimwenguni WHO, kwenye kikao kilichoandaliwa na kamati ya Afya ya shirika hilo mjini Brazaville nchini Congo Jumanne .

Ndugulile alizoa kura 25 kati ya zote 46 akiwashinda wapinzani wa kutoka Rwanda,Niger na Senegal huku akipata uungwaji mkono kwa mataifa 25 ikiwemo Kenya.

Waziri huyo mdogo wa zamani wa Afya nchini Tanzania anamrithi Dkt Matshidiso Rebecca Moeti wa Botswana, aliyekamilisha muda wake wa mihula miwili.

Dkt Ndugulile ni Mbunge wa eneo bunge la Kigamboni jijini Dar es Salaam na pia ni naibu mwenyekiti wa kamati ya bunge kuhusu afya na virusi vya ukimwi nchini Tanzania.

Share This Article