Mtandao wa kampuni ya Mookh.com iliyojukumiwa kuuza tiketi za robo fainali kuwania kombe la CHAN kati ya Kenya na Madagascar Ijumaa hii umedukuliwa.
Kulingana na taarifa kutoka kwa kampuni hiyo mtandao huo ambao ulikuwa uanze kutumika kuuza tiketi hizo kuanzia saa sita adhuhuri leo ulikwama kutokana na kudukuliwa.
Imedaiwa kuwa kumekuwa na maroboti mengi yaliyojazwa katika mtandao huo ili kununua tiketi, hali inayowanyima mashabiki halisi fursa ya kununua tiketi.
Mookh.com imesikitishwa na kuporomoka kwa mtandao huo na kuahidi kurekebisha hali.
Kenya itapambana na Madagascar, Ijumaa hii kuanzia saa kumi na moja jioni katika uwanja wa Kasarani katika robo fainali ya kwanza.