Mswada wa kuongeza muda wa urais kutoka miaka 5 hadi 7 kuwasilishwa Seneti

Dismas Otuke
1 Min Read

Seneta wa kaunti ya Nandi Samson Cherargei ameandaa mswada wa kubadilisha katiba ili kuongeza muda wa kuhudumu wa Rais kutoka miaka mitano hadi saba.

Mswada huo unatarajiwa kuwasilishwa na kusomwa hivi karibuni katika bunge la Seneti.

Unapendekeza kuongeza muda wa kuhudumu wa Rais, Magavana, Maseneta, Wabunge, Mwakilishi wa Kina Mama na Mwakilishi Wadi hadi miaka saba badala ya mitano.

Awali,  mbunge wa Fafi Salah Yakub aliwasilihsa mswada wa kupendekeza kuondolewa kwa muda wa kuhudumu na badala yake kuweka umri wa miaka 75 kwa viongozi wote wanaochaguliwa lakini mswada huo ukakataliwa mbali.

Mswada wa Seneta Cherargei huenda ukazua tumbo joto na mhemko mkubwa kutoka kwa Wakenya ambao wana maoni kinzani na hasa kuhusiana na bunge hilo la Seneti.

Share This Article