Msumbiji kuomboleza Papa Francis kwa siku tatu

Jared Ombui
1 Min Read
Papa Francis.

Serikali ya Msumbiji imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kuanzia Alhamisi, tarehe 24 Aprili 2025, kwa heshima ya Papa Francis, aliyefariki dunia Jumatatu mjini Vatican.

Uamuzi huo ulifikiwa wakati wa mkutano wa 13 wa Baraza la Mawaziri, uliofanyika Maputo.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kikao hicho, Waziri Salimo Valá alieleza kuwa uamuzi wa serikali umetokana na kutambua unyenyekevu wa Papa Francis, kujitolea kwake kwa ajili ya waliotengwa na juhudi zake za kutafuta amani.

Katika kipindi cha maombolezo ya kitaifa, bendera ya taifa na bendera ya rais zitapeperushwa nusu mlingoti kote nchini na katika balozi na ofisi za kibalozi za Msumbiji.

Papa Francis aliitembelea Msumbiji Septemba 2019.

Share This Article