Msomaji habari wa zamani katika runinga ya KTN Njoroge Mwaura ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 74.
Kulingana na mkewe Lucy Mwaura, marehemu amekuwa akipokea matibabu katika hospitali moja jijini Nairobi, na hali yake ilidorora kuanzia Jumamosi usiku baada ya kufanyiwa upasuaji.
Njoroge alifariki baada ya kukimbizwa katika chumba cha wagonjwa mahututi .
Marehemu alianzia taaluma yake ya usomaji habari kwenye televisheni ya KBC, kabla ya kujiunga na KTN hadi alipostaafu mwaka 2012.
Mwendazake Njoroge amemwacha mjane na watoto wanne.