Maafisa wa polisi wamemkamata mshukiwa wa ulanguzi wa mihadarati katika kaunti ya Kwale.
Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai DCI, imesema kuwa maafisa hao kutoka katika kituo cha polisi cha Samburu, walimkamata mshukiwa huyo kwenye Barabara Kuu ya Nairobi-Mombasa akisafirisha mihadarati hiyo akitumia gari aina ya Mazda CX-5 lenye nanbari za usajili KDR 284H.
Kulingana na idara hiyo, Christopher Hannington Jobita alipatikana na magunia kadhaa ya bangi kwenye gari hilo.
Mshukiwa huyo alipelekwa kwenye kituo cha polisi cha Samburu, akisubiri kufikishwa mahakamani.
Bangi hiyo na gari hilo, zinazuiliwa kama Ushahidi, huku polisi wakianzisha msako dhidi ya washirika wa mshukiwa huyo walio mafichoni.