Maafisa wa idara ya kukabiliana na ulanguzi wa mihadarati nchini (ANU), wamemkamata mshukiwa wa ulanguzi wa mihadarati, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA).
Muli Ayan Ndunge mwenye umri wa miaka 34, aliyekuwa amemeza dawa hizo za kulevya, alikamatwa muda mfupi baada ya kutua katika uwanja huo wa ndege kutoka Jijini Addis Ababa,Ethipoia.
Baada ya maafisa wa ANU kumfanyia uchunguzi kutumia mashini za xray, walipata vipande 28 vya dawa ya kulevya aina ya cocaine zenye uzani wa gramu 912.74 za gharama ya shilingi 3, 650, 960.
Kwa sasa Ndunge anazuiliwa na maafisa wa polisi, akisubiri kufikishwa mahakamani.