Polisi kutoka eneo la Nairobi wamemkamata mshukiwa wa ulanguzi wa dawa za kulevya na kunasa kiwango kikubwa cha bangi.
Mshukiwa huyo alikamatwa wakati wa operesheni kali iliyofanyika katika eneo la Umoja 1 Market, kaunti ndogo ya Buruburu.
Huduma ya Taifa ya Polisi, NPS inasema wakati wa operesheni hiyo, maafisa walinasa kilo zipatazo 20 za bangi pamoja na misokoto 3,ooo ambayo tayari ilikuwa imetayarishwa.
Aidha, vifurushi 33 vya dawa hiyo ya kulevya vilinaswa na vitatumiwa kama ushahidi mshukiwa atakapofikishwa mahakamani.
NPS imeimarisha msako dhidi ya dawa za kulevya nchini katika siku za hivi karibuni.