Mshukiwa wa ugaidi akamatwa Nairobi

Jamaa huyo alipatikana na vifaa vinavyoaminika kuwa vilipuzi.

Marion Bosire
1 Min Read

Mshukiwa wa ugaidi alikamatwa na maafisa wa polisi jijini Nairobi usiku wa Jumatatu tarehe 17 mwezi Juni mwaka huu wa 2025.

Polisi hao wa kituo cha polisi cha Kamukuji walikuwa wakishika doria kama kawaida walipokumbana na jamaa huyo saa tano na dakika ishirini hivi.

Tabia aliyodhihirisha jamaa huyo ya kutaka kukwepa maafisa hao wa usalama na kutokuwa na uhakika ilisababisha wamchunguze zaidi wakitaka kujua alichokuwa amebeba.

Waliposaka mzigo wake, maafisa hao walipata vilipuzi 21, pakiti 21 za kitu kinachoaminika kuwa kemikali ya ammonium nitrate, waya wa urefu wa mita tano na vitu vingine.

Maafisa hao walimkamata jamaa huyo na baadaye kumwasilisha kwa maafisa wa kitengo cha kukabiliana na ugaidi – ATPU kwa uchunguzi na hatua zaidi.

Share This Article