Maafisa wa kukabiliana na ugaidi (ATPU), wamemkamata Asho Kassim Hassan, anayedaiwa kusaidia kundi moja la kigaidi.
Alikamatwa baada ya maafisa hao kutekeleza operesheni iliyowapeleka hadi kwenye maficho yake mtaani Eastleigh.
Maafisa hao walipata pasipoti na simu ya rununu ambazo kwa sasa zinafanyiwa uchunguzi wa kisayansi ili kutambua mtandao ambao anahusishwa nao.
Kwa sasa mshukiwa huyo anazuiliwa kwenye korokoro za polisi, akisubiri kufikishwa mahakamani.
Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai kupitia ukurasa wa X, ilisema operesheni hiyo ilifanikishwa na ushirikiano wa hali juu na asasi zingine za usalama na jamii.