Maafisa wa polisi wa kituo cha polisi cha Mbale walitekeleza msako mkali jana, Agosti 18, 2025 katika eneo la Mbihi ambapo walilenga walanguzi wa mihadarati.
Katika operesheni hiyo, maafisa walifanikiwa kukamata mshukiwa mmoja wa kike aliyepatikana akiwa na mafungu 15 ya bangi kwenye barabara ya Mbihi.
Mwanamke huyo amezuiliwa katika kituo hicho cha polisi akisubiri uchunguzi zaidi kabla ya kufikishwa mahakamani, huku huduma ya taifa ya polisi ikiimarisha juhudi za kukabiliana na ulanguzi na matumizi ya mihadarati kote nchini.