Mshukiwa mkuu wa mauji ya Were alimfuata kutoka nje Bunge

Tayari dereva na mlinzi wa marehemu wamehojiwa na maafisa wa polisi pamoja na mwenye duka la MPESA ambapo dereva wa marehemu alifanya muamala.

Dismas Otuke
1 Min Read
Mbunge wa Kasipul Charles Ong’ondo Were.

Majasusi wanaendelea kuunganisha vyanzo kadhaa ili kumtambua mshukiwa mkuu wa mauaji ya Mbunge wa Kasipul Charles Ong’ondo Were Aprili 30.

Kamera za CCTV zinaashiria kuwa mshukiwa huyo aliyekuwa amefunika uso akiwa na mwendesha pikipiki walionekana wakifuata gari la mbunge huyo katika kila hatua kutoka nje ya bunge, kuingia katikati ya jiji, hadi barabara ya Valley na hatimaye katika mzunguko wa barabara ya Ngong ambapo mshukiwa mkuu alimfyatulia risasi tano mbunge huyo.

Tayari dereva na mlinzi wa marehemu wamehojiwa na maafisa wa polisi pamoja na mwenye duka la MPESA ambapo dereva wa marehemu alifanya muamala.

Aidha, polisi wamewataka wananchi walioshuhudia kisa hicho kutoa taarifa zitakazosaidia kumtia mbaroni washukiwa.

Share This Article