Moto wateketeza mali Kariobangi

Dismas Otuke
0 Min Read

Mali ya thamani isiyojulikana imeteketea Jumapili alasiri kwenye mkasa wa moto mtaani Kariobangi, kaunti ya Nairobi.

Yasemekena moto huo ulianzia katika duka moja la kuuza mbao.

Maafisa wa zimamoto wa kaunti ya Nairobi, waliwasili mahali hapo na kufanikiwa kuuzima moto huo uliokuwa umeharibu mali ya mamilioni ya pesa.

Chanzo cha moto huo hakijabainika kufikia sasa.

Share This Article