Moto waripotiwa katika shule ya Katoloni kaunti ya Machakos

Marion Bosire
1 Min Read

Kisa cha moto kiliripotiwa usiku wa kuamkia leo katika shule ya sekondari ya Katoloni katika kaunti ya Machakos.

Shirika la msalaba mwekundu nchini liliripoti kwamba shughuli ya kuzima moto huo zilikuwa zinaendelea. Kulingana na shirika hilo, moto huo ulizimwa kwa ushirikiano kati ya wafanyakazi wake na wazima moto wa kaunti ya Machakos.

Shirika hilo lilianzisha pia shughuli ya kutoa usaidizi na huduma ya kwanza wa walioathirika.

Chanzo cha moto huo hakijabainika na kufikia sasa hakuna taarifa kamili kuhusu walioathiriwa na moto huo. Maafisa wa usalama wa eneo hilo waliomba wakazi wa maeneo ya karibu na shule ya Katoloni kutokusanyika humo.

Wazazi na walezi wa wanafunzi wa shule hiyo pia wameombwa wasalie watulivu.

Share This Article