Moto mkubwa wateketeza afisi za Chuo Kikuu cha Tharaka

Martin Mwanje
1 Min Read

Moto mkubwa ulizuka usiku katika Chuo Kikuu cha Tharaka na kuteketeza afisi kuu ya chuo hicho. 

Wakazi wa eneo hilo wamekosoa vikali serikali ya kaunti kwa kile walichokitaja kama uzembe katika kukabiliana na mkasa huo.

Kwa mujibu wa Naibu Chansela wa chuo hicho, Prof. Kinyua Muriungi, shughuli za kila siku zikiwemo masomo zinaendelea kama kawaida licha ya mkasa huo.

Ameeleza kuwa hakuna majeruhi walioripotiwa na usalama wa wanafunzi uko thabiti.

Mkuu wa eneo la Tharaka Kusini Stephen Mavina amesema uchunguzi wa kina unaendelea ili kubaini chanzo halisi cha moto huo.

Aidha, amewataka wakazi pamoja na wanafunzi kuwa watulivu na subira wakati uchunguzi ukiendelea.

Share This Article