Mfalme Mohammed wa sita wa Morocco, jana amezindua ujenzi wa reli ya kisasa ya mwendokasi ya umbali wa kilomita 430 mjini Rabat inayounganisha Kenitra-Marrakech, itakayogharimu shilingi trilioni 1.3 za Kenya.
Reli hiyo mpya itaunganisha miji ya Rabat, Casablanca na Marrakech na kuunganisha viwanja vya ndege vya Rabat na Casablanca.
Ujenzi wa reli hiyo utagharimu shilingi bilioni 739, huku kiwango kingine cha shilingi bilioni 404.5,kikitumika kununua treni 168 za mwendokasi .
Treni hizo mpya zikikamilika zitachukua muda wa saa moja kusafiri kutoka mjini Tangier hadi mjini Rabat, saa 1 na dakika 40 kutoka mjini Tangier hadi Casablanca na saa 2 na dakika 40 kutoka Tangier hadi Marrakech na kuokoa muda wa saa mbili.