Morocco ndiyo timu ya pili kutoka Afrika kunyakua Kombe la Dunia kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 20, baada ya kuwalaza Argentina mabao 2-0, katika fainali iliyosakatwa mapema leo mjini Santiago, Chile.
Yassir Zabiri alipachika magoli hayo mawili katika dakika za 12 na 29 na kuifanya Morocco kuwa nchi ya pili ya Afrika kunyakua kombe hilo la wanaume tangu Ghana kufanya hivyo mwaka 2009.
Ushindi wa Morocco unafuatia timu ya taifa ya Atlas Lions kumaliza ya nne na kuwa ya kwanza kutoka Afrika kufikia nusu fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar.