Morocco wapiga mazoezi ya kwanza baada ya kuwasili Kenya

Morocco ambao watafungua dimba kundini A Jumapili hii dhidi Angola katika uwanja wa Nyayo walikuwa wa  kwanza kutua Kenya jana Alfajiri.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa mara mbili wa kombe la Afrika kwa wachezaji wa Ligi za nyumbani (CHAN), Morocco walifanya mazoezi ya kwanza katika uwanja wa Kasarani Annex, jana usiku baada ya kuwasili mapema asubuhi.

Morocco ambao watafungua dimba kundini A Jumapili hii dhidi Angola katika uwanja wa Nyayo walikuwa wa  kwanza kutua Kenya jana Alfajiri.

Kikosi cha Morocco kinawajumuisha wachezaji kutoka vilabu vya FUS Rabat, ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu; RS Berkane, walioshinda kombe la shirikisho; Raja Casablanca; na Wydad Casablanca.

Simba hao wa milima ya Atlas wanarejea CHAN mwaka huu baada ya kujindoa kwa makala ya mwaka 2022 nchini Algeria kufuatia mzozo wa kidiplomasia kati ya Algeria na Morocco.

Share This Article