Morocco inatarajiwa kuanza ujenzi wa uwanja wa Sidi Slimane mjini Benslimane, utakaomudu mashabiki 115,000, kwa gharama ya shilingi bilioni 41.2 za Kenya .
Uga huo ambao utakuwa mkubwa zaidi Afrika punde utakapokamilika unatarajiwa kukamilishwa ifikiapo mwaka 2027 ,tayari kwa maandalizi ya fainali za Kombe la Dunia mwaka 2030.
Uwanja huo wa kisasa utajumuisha uwanja wa riadha unaoselehi mashabiki 25,000, na utafikika kwa urahisi kutoka miji ya Rabat,Casablanca na Benslimane kupitia kwa usafiri wa angani,reli na barabara za kisasa.
Morocco itautumia uga huo kuandaa kipute cha Kombe la Dunia kwa pamoja na Uhispania na Ureno mwaka 2030.