Monsuru Ayanfe asimulia kuhusu wema wa Funke Akindele

Alimkosea mwigizaji huyo ambaye alikasirika mara ya kwanza kabla ya kubadili na kuwa mkarimu.

Marion Bosire
1 Min Read

Mwigizaji wa filamu za Nollywood nchini Nigeria Ayanfe Monsuru amesimulia kuhusu wema wa mwigizaji mwenza ambaye pia ni mwandalizi wa filamu Funke Akindele uliomshangaza.

Akizungumza kwenye mahijiano Ayanfe alisimulia kuhusu kisa kilichotokea wakati mmoja wakiwa katika eneo la maandalizi ya filamu na Akindele.

Ayanfe alisema alijukumiwa kuegesha gari la Funke Akindele na alipokuwa akifanya hivyo, anasema aligongesha gari hilo analolitaja kuwa jipya.

Kulingana na mwigizaji huyo, Funke Akindele hakufurahishwa na hilo na akawa amejawa na ghadhabu.Baadaye hata hivyo Funke alimwomba msamaha kwa kumfokea punde baada ya kisa hicho kutokea.

“Mimi ndio nilikuwa na makosa. Niligongesha gari lake jipya lakini baadaye aliniomba msamaha.” Alisema Monsuru kwenye mahojiano hayo.

Anamwelezea Funke kama mtu anayekasirika haraka lakini ni mkarimu.

Olufunke Ayotunde Akindele ambaye anafahamika na wengi kama Funke Akindele wa umri wa miaka 47 sasa amekuwa kwenye ulingo wa uigizaji nchini Nigeria amekuwa akiigiza tangu mwaka 1998.

Alijipatia umaarufu alipoigiza kwenye kipindi cha vichekesho kilichokuwa kikifahamika kama “I Need to Know” kilichokuwa kinafadhiliwa na shirika la umoja wa mataifa kuhusu idadi ya watu UNFPA.

Amesomea shahada ya uanasheria katika chuo kikuu cha Lagos baada ya kusomea stashahada ya uanahabari katika taasisi ya mafunzo ya kiufundi ya jimbo la Ogun.

Share This Article