Mohammed Iqbal Dar, aliyebuni jina Tanzania ameaga dunia nchini Uingereza akiwa na umri wa miaka 80.
Dar, ambaye alihamia nchini Uingereza alifariki baada ya kuugua kwa muda wa takriban miaka 10, ugonjwa uliomsababisha kushindwa kutembea.
Iqbal Dar ambaye ni wa jamii ya Kiislamu ya Ahmadiyya, alikuwa miongoni mwa kundi la watu lililokuwa likijadili kuunganishwa kwa Tanganyika na Zanzibar kuwa taifa moja.
Ni katika majadiliano hayo ambapo pendekezo la Dar la jina ‘Tanzania’ lilikubalika, jina hilo likuwa kuunganishwa kwa jina Tanganyika na Zanzibar.
Dar aliona tangazo kwenye gazeti moja kuhusu shindalo la kutafuta jina jipya baada ya kuunganishwa kwa Tanganyika na Zanzibar.
Akiwa mwanafunzi katika shule ya upili ya Mzumbe, aliwasilisha jina ‘Tanzania’ na likaibuka mshindi, huku akituzwa shilingi 200 na medali.
Alikabidhiwa tuzo hiyo na waziri wa habari Sheikh Idrisa Abdul Wakil.
Dar atakumbukwa daima katika historia ya Tanzania.