Mkutano wa pamoja wa EAC, SADC juu ya DRC wafanyika Ikulu

Martin Mwanje
1 Min Read
Rais William Ruto (kulia) akiwa na mwenzake wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa

Mkutano wa wenyeviti wenza wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unafanyika leo Ijumaa katika Ikulu ya Nairobi.

Mkutano huo unahudhuriwa na mwenyeji wake, Rais William Ruto ambaye pia ni mwenyekiti wa EAC na Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ambaye pia ni mwenyekiti wa SADC.

Wote hao wanakutana na Jopo la Wapatanishi wa Mchakato wa Amani wa DRC, akiwemo Rais mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Mkutano huo unakuja siku moja baada ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) na Rwanda kufanya mazungumzo yao ya kwanza tangu kutia saini makubaliano ya amani ya kumaliza mgogoro uliodumu miongo kadhaa.

Mgogoro huo umeikumba mashariki ya DRC ambayo ina utajiri mkubwa wa madini.

Mataifa hayo mawili yalisema leo Ijumaa kuwa mazungumzo kati yao yameng’oa nanga.

“Julai 31, 2025, wawakilishi kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) na Jamhuri ya Rwanda (Rwanda), pamoja na waangalizi” walifanya mkutano wao wa kwanza mjini Washington tangu kutiwa saini kwa makubaliano ya amani katika mji huo mkuu wa Marekani Juni 27,” ilisema taarifa ya pamoja iliyotolewa na mataifa yote mawili kwenye mitandao ya kijamii leo Ijumaa.

Share This Article