Mkutano mkuu wa mwaka wa kamati ya kitaifa ya Olimpiki NOC-K, umeanza leo jijini Nairobi huku ajenda kuu ikiwa uchaguzi wa viongozi.
Hata hivyo ajenda kuu ya mkutano huo ambayo ni uchaguzi wa viongozi inasubiri mwelekeo wa mahakama.
Mahakama ya kutatua migogoro michezoni, SDT imeamuru kuwa mashirikisho ya Taekwondo, Voliboli na Uogeleaji yameruhusiwa kupiga kura.
Kizungumkuti kinachokabili uchaguzi wa leo ni kesi ya SDT ya kuamuru ni nani kati ya wenyeviti wa mashirikisho ya michezo Makatibu wao wataruhusiwa kupiga kura.