Mkewe Rais ahimiza usaidizi kwa mtoto wa kike

Alizungumza katika maadhimisho ya siku ya kufikiria ulimwenguni na miaka 105 ya shirika la Kenya Girl Guides.

Marion Bosire
2 Min Read

Mke wa Rais William Ruto Bi. Rachel Ruto, amehimiza juhudi za pamoja katika kusaidia watoto wa kike ili waweze kuafikia kikamilifu uwezo wao katika maisha.

Mama taifa alitaja umasikini uliokithiri kuwa mojawapo ya vikwazo vikuu kwa safari ya wasichana ya kuafikia ndoto zao huku wengi wakilazimika kubeba mzigo wa kusaidia wazazi wao katika kuhudumia familia.

Kulingana naye, hakuna juhudi zinafaa kuachwa katika kuhakikisha kila msichana anaweza kupata elimu na huduma nyingine muhimu za kumpa ujuzi wa kubadili maisha yake na kumwezesha kuchangia maendeleo ya nchi.

Alikuwa akizungumza katika maadhimisho ya mwaka huu ya siku ya kufikiria ulimwenguni, katika changamano la Moi huko Nyeri katika maadhimisho ya miaka 105 tangu kuanzishwa kwa shirika la Kenya Girl Guides.

Rachael Ruto alisema mkakati wa kuafikia lengo la serikali ya mpito wa asilimia 100 wa wanafunzi kutoka kiwango kimoja cha elimu hadi kingine, ni kuhakikisha Kenya inatimiza lengo la kuhakikisha watoto milioni 10 wanapata chakula kufikia mwaka 2030.

Mama taifa alitoa changamoto kwa taasisi za elimu kusaidia shirika la Girl Guides katika kuafikia sukuhisho tekelezi zinazoweza kusaidia kukabiliana na changamoto zinazokumba taifa kama mabadiliko ya tabianchi na ukosefu wa chakula cha kutosha.

Alisema iwapo mafunzo yatatolewa na usaidizi kutoka kwa makundi kama 4K club, shirika hilo linaweza kubadili jamii kwa kuandaa mipango itakayoleta mabadiliko kote nchini.

Share This Article