Mkewe Kikwete na mwanawe Magufuli kuwania ubunge kwa chama cha CCM

Tanzania itashiriki uchaguzi wa udiwani, ubunge, na urais Oktoba 28 mwaka huu.

Dismas Otuke
0 Min Read
Salma Kikwete, mkewe Rais Mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete

Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania kimemteua mwanawe Rais wa awamu ya tano Hayati John Pombe Magufuli, Jessica Magufuli, kugombea Ubunge wa Viti maalum kupitia kundi la UVCCM.

Aidha, CCM kimemteua Salma Kikwete, mkewe Rais mstaafu Jakaya Kikwete, kuwa mgombea pekee wa ubunge jimbo la Mchinga, mkoani Lindi.

Jessica Magufuli

Tanzania itashiriki uchaguzi wa udiwani, ubunge, na urais Oktoba 28 mwaka huu.

 

Share This Article