Misri ilikuwa timu ya tatu ya Afrika kujikatia tiketi kwa fainali za 23, za Kombe la Dunia mwaka 2026 baada ya kuwalaza Djibouti mabao 3-0, katika mechi iliyopigwa mjini Casablanca,Morocco.
Mohammed Salah alipachika mabao 2 huku Ibrahim Adel akiongeza moja huku Misri wakiongoza kundi A kwa pointi 23.
Misri wanajiunga na Morocco na Tunisia ambao wamejikatia tiketi kwa fainali za mwaka ujao zitakazoandaliwa kwa pamoja na Marekani,Canada na Mexico.
Ni mara ya nne kwa Mafarao hao kufuzu kwa Kombe la Dunia baada ya kushiriki makala ya 1934, 1990 na 2018.