Migawanyiko Muumbuni Kaskazini, Machakos kuelekea uchaguzi mdogo

Martin Mwanje
1 Min Read
Kinara wa Wiper, Kalonzo Musyoka akihutubia mkutano wa awali

Chama cha Wiper na vyama vinavyounga mkono siasa za upinzani katika kaunti ya Machakos vimeombwa kuwa na mgombea mmoja katika uchaguzi mdogo wa wadi ya Muumbuni Kasikazini ili kuibuka mshindi kwenye kinyang’anyiro hicho.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa chama cha KANU, tawi la Machakos Petet Thuva, akizungumza baada ya kutangaza kuwa chama cha KANU kitaunga mkono mgombea wa chama cha Wiper kwenye uchaguzi huo, amekitaka chama cha Chama cha Uzalendo (CCU) kumwomdoa mgombea wake kwenye uchaguzi huo.

Kulingana na Thuva, kuwepo kwa wagombea wengi kwenye vyama vya upinzani kutasababisha chama cha Wiper kuwa na nafasi finyu ya kushinda kwenye uchaguzi huo na kuvipa vyama vya UDA na Maendeleo Chap chap nafasi za juu kushinda uchaguzi huo mdogo.

Chama cha Uzalendo kinachohusishwa na Gavana Wavinya Ndeti mwishoni mwa juma kilimtangaza mgombea wake kwenye uchaguzi huo na kuibua hisia za uwepo wa migawanyiko miongoni mwa wafuasi wa kinara wa Wiper, Kalonzo Musyoka.

Share This Article